
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amehudhuria katika msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mwanasiasa mkongwe Augustine Lyatonga Mrema aliyefariki wakati akifanyiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sambamba na kutoa salamu za rambirambi Dkt Mpango amewataka wafiwa kuwa na subra katika wakati huu mgumu huku akiwaomba wawe wajasiri kutokana na kuondokewa na mpendwa wao.

Aidha Makamu wa Rais amemuongelea marehemu kama mtu aliyekuwa muadilifu na mzalendo kwa Taifa lake ambaye alifanya kazi zake kwa uadilifu katika nyadhfa mbalimbali alizopewa serikalini.