
Serikali, Bw. Alfred Shao wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kutengeneza mfumo wa kidijitali wa kutunza
taarifa za Diaspora.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB wamesaini Hati ya Makubaliano ya
kutengeneza Mfumo wa Kidigitali, (Diaspora Digital Hub System) ambapo benki hio imedhamini Shilingi Milioni 100
ili kuboresha huduma za mfumo huo zenye kukidhi mahitaji ya Diaspora.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Mhe. Balozi James Bwana alisema mfumo huo wa kidigitali utaisaidia Serikali
kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania waliopo sehemu mbalimbali ulimwenguni kupata
huduma mbalimbali ikiwemo za kibenki na kushiriki kidigitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, biashara,
uchumi na uwekezaji nchini.

Lakini pia, itafungua uwezekano wa fursa zaidi na kufahamu kwa ufasaha idadi ya Diaspora, ujuzi, elimu na
wenyewe wataweza kupata huduma mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Bw. Alfred Shao alisema kuwa wanaamini
kukamilika kwa mfumo huo kutawawezesha Diaspora wa Tanzania kuungana, kutambulika na kuiwezesha Serikali
kuwa na Kanzi Data ya uhakika na kuwafikia diaspora wengi kwa wakati mmoja na hivyo kuleta mafanikio
makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja anayeishi nje ya nchi.

Mhe. Balozi James Bwana katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kusainiwa kwa
Hati ya makubaliano jijini Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Mhe. Balozi James Bwana kwa niaba,
Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Bw. Alfred Shao na kushuhudiwa na Kaimu Katibu wa Bodi ya
Wakurugenzi wa NMB, Consolatha Mosha na Mwanasheria wa Wizara – Miriam Kilo katika Ofisi Ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam.