×

Bilionea Elon Musk: Kuna Upungufu Mkubwa wa Watu Wanaozaliwa Duniani

Elon Musk

ELON MUSK; ni tajiri namba moja duniani mwenye utata mkubwa kutokana na kauli zake zisizoeleweka mbele wala nyuma kama kitumbua ambaye kwa mara nyingine tena amezua mjadala mkali huko Twitter.

 

Musk bila kutetereka ametoa msimamo wake kwa kusema kwamba watu wamekuwa wazembe katika uzazi na kutozaa watoto wengi ni athari kubwa katika ulimwengu kuliku athari za tabia ya nchi kwa kimombo global warming.

 

Musk anasema kuwa, watu wengi wanaamini athari za tabia ya nchi ndiyo athari kubwa kabisa itakayokumba mataifa mengi katika miaka michache ijayo, lakini amelipinga hilo kwa kusema kwamba watu kutozaana ndilo litakuwa tatizo kubwa.

 

“Kuna kuporomoka kwa idadi ya watu kutokana na viwango vya chini vya kuzaliwa, ni athari kubwa zaidi kwa ustaarabu kuliko ongezeko la joto duniani na tabia ya nchi, zingatia maneno haya yangu,” anasema Musk.

Idadi ya watu imepungua Duniani kwa mujibu wa Elon Musk

Watu wengi duniani wamekumbatia mfumo wa uzazi wa mpango ili kujaribu kudhibiti idadi ya watoto wanaozaliwa kutokana na hali ya uchumi kuzorota na gharama ya maisha kupanda kila uchao.

 

Wengi wanapinga vikali kauli hii ya Musk ya kuwataka watu kuzaana kwa wingi ili uepusha kile alichokiita athari ya kutokomea kwa ustaarabu kutokana na idadi ndogo ya watu wanaozaliwa na wengi wakizidi kutangulia mbele za haki.

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment