×

Washindi wa M Pesa Imeitika Walivyokabidhiwa Bodoboda na Bajaj, Nyumba Yasubili Mshindi

Washindi wa bodaboda baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

 

 

KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom Agosti 26 mwaka huu imewakabidhi zawadi zao washindi wa promosheni ya M Pesa Imeitika inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa wateja wake ambapo washindi watatu walikabidhiwa bodaboda walizojishindia na mmoja aliondoka na Bajaj. Washindi hao hupatikana kila wiki.

Mkuu wa Vodacom Kanda ya Mashariki na Pwani, Birgita Shirima (kulia) akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa Bajaj, Magdalena Magoma.

 

 

Akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa zawadi hizo iliyofanyika Viwanja vya Barafu vilivyopo Mburahati jijini Dar, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Mashariki na Pwani, Birgita Shirima alisema lengo la promosheni hiyo ni kuishukuru serikali kwa kusikia kilio cha Watanzania wengi na kurekebisha suala la tozo. Aliendelea kusema;

 

“Kwanza kabisa tunatoa shukrani kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wake Mama Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha wengi na kufanya mabadiliko ya tozo ndiyo maana nasi kupitia kampeni yetu hii ya M Pesa imeitika nasi tumeamua kuoresha maisha ya wateja wetu na kuwapa huduma bora zaidi.

Mkuu wa Vodacom Kanda ya Mashariki na Pwani, Birgita Shirima (kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa Bajaj, Magdalena Magoma.

 

“Leo hapa kuna wateja wetu wataondoka na Bajaj na bodaboda walizojishindia kupitia promosheni hii. Hivyo basi tunawashauri Watanzania watumie huduma za M Pesa ambapo ukifanya mualama wowote kupitia huduma ya M Pesa unakuwa umeingia kwenye kinyanganyiro cha zawadi hizi”. Alisema.

Mwanamuziki wa singeli, Dullah Makabila akinogesha mambo kwenye hafla hiyo.

 

Birgita alimaliza kwa kusema pamoja na zawdi hizo kuna zawadi ya nyumba ya kisasa yenye fenicha za kisasa kutoka kampuni ya GSM.

Leave a Comment