
KATIKA kutoa fundisho na kukomesha vitendo vya kishirikina vinavyobabisha migogoro ya kifamilia na Jamii na kupelekea mauaji mwendesha mashtaka wa Serikali aliiomba Mahakama kumpatia mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Baada ya mapendekezo hayo ya mwendesha mashtaka hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela Mzee John Sevelini Chale (60) wa Kijiji cha Iwela Wilayani Ludewa kwa kosa la kukutwa na hatia ya uchawi kwa kumfanya mtoto wa mdogo wake anayejulikana kwa jina la Vediana Chale kuwa kichaa.

Mzee John Sevelini Chale alikutwa na hatia baada ya kukutwa na kosa la kujihusisha na vitendo vya kishirikina kinyume na kifungu cha 3(a) na 5(1) cha sheria ya uchawi sura ya 18 marejeo 2019.
Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.