
MTANZANIA anayeishi nchini Ubelgiji Sophie Ledani ambaye ni mwanzilishi wa Foundation ya Samaritan VZW Belgium ambayo inasaidia watu wwenye changamoto mbalimbali ikiwemo Watoto wa kike waliokatishwa masomo kutokana na kupewa ujauzito, wanawake wagonjwa, wazee, walemavu pamoja na Shule zenye uhitaji kama vile vyoo, visima na mahitaji mengine ya masomo.
Katika kufanikisha hilo Bi. Sophie aliweza kufanya tukio maalum la harambee ambalo liliendana na kuuza baadhi ya bidhaa kutoka Tanzania pamoja na kuandaa chakula maalum cha kitanzania kwa ajili ya wageni ili kuweza kutengeneza pesa za kutoa misaada nchini Tanzania.

Aidha Bi. Sophie amesema kuwa adhima yake kuu ni kuunga juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia Watanzania hasa wale walio katika mazingira magumu.
Katika harambee yake anatarajiwa kupeleka mapato yake moja kwa moja kwa makundi yaliyoainishwa kama ilivyo lengo mama la Foundation hiyo na kwa kuanzia anakwenda kutoa msaada katika Shule ya Msingi Nkurumo iliyopo nchini Tanzania