×

Watu 15 Wauawa kwa Kupigwa Risasi Katika Vurugu za Baghdad

Kiongozi wa Siasa nchini Iraq Mogtadal Al Sadr

WAFUASI 15 wa Ulamaa wa kidini katika dhehebu la Shia nchini Iraq wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano yaliyofanyika katika maeneo yaliyopo karibu na Ikulu ya Rais nchini humo.

 

Makabiliano hayo yalifanyika katika majengo ya serikali yaliyopo Mji wa Baghadad na kusababisha takribani waandamanaji 350 kujeruhiwa kwa risasi na wengine kuvuta gesi ya mabomu ya machozi.

 

Hayo yamejiri baada ya kiongozi wa siasa nchini Iraq, Moqtada al-Sadr kujiuzulu katika masuala ya kisiasa hatua  iliyochochea wafuasi wake kuvamia eneo la majengo ya serikali yenye ulinzi mkali, ambapo kunapatikana balozi tofauti, katikati mwa Mji Mkuu wa Iraq, Baghdad.

Vurugu mjini Baghdad

Sadr anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye nguvu zaidi nchini Iraq na amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kuhusu kuunda serikali.

 

Maandamano yalienea katika maeneo mengine ya nchi, huku wafuasi hao wakivamia majengo ya serikali katika miji mbalimbali ukiwemo wa Kusini mwa nchi hiyo.

Vurugu zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 15

Mivutano ya kisiasa imeongezeka nchini Iraq na kusababisha mzozo wa kisiasa ambao umechangiwa na kushindwa kuundwa kwa serikali mpya kwa miezi kadhaa.

 

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment