
MKUU wa wlilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameipongeza kampuni ya simu ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta mapinduzi ya maendeleo ya tekhnolojia yanayosaidia jamii.
Gondwe aliyasema hayo siku ya tarehe 29 mwezi huu alipotembelea washindi wa bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M pesa imeitika, alisema kuwa Vodacom wamekuwa vinara katika kuleta mapinduzi ya technolojia na huduma zinazonufaisha watanzania wote.

“Vodacom imeweza kuwa ya kwanza kwa M PAWA, Vodacom imekuwa ya kwanza kuleta M MAMA inayosaidia kina mama kufika hospitalini na kupata huduma kwa haraka ni jambo kubwa sana, lakini pia Vodacom wameweza kuleta 4G kwa hiyo sisi kama serikali tunawapongeza sana”.
Nao washindi wa zawadi za bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M pesa imeitika ambao ni Magdalena Magoma na Beata Madachi wameishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoiwezesha kampuni ya Vodacom kufanya kazi kwa urahisi nchini kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote.
Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.