
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametaja sababu zinazofanya Jeshi la Polisi kuwa legelege kuwa ni upungufu wa mafunzo ndani ya Jeshi hilo.
Rais Samia ameyasema hayo siku ya Jumanne Agosti 30, 2022 katika ufunguzi wa kikao kazi cha Maofisa Wakuu Waandamizi wa Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi na vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania (TPS) mkoani Kilimanjaro.

“Tathimini yetu ni kwamba upungufu wa mafunzo unalifanya Jeshi la Polisi maeneo mengine liwe limelegea au kuwepo na mmomonyoko wa maadili ndani ya Jeshi” alisema Rais Samia.
Pia aliongezea kwa kusema kuwa kuajiri Polisi wasiokuwa na vigezo ikiwemo wale wanaoshindwa vyuoni ndiyo sababu inayolitia Jeshi la Polisi aibu, kwa sababu Polisi hawa wamekuwa wakirekodiwa mtandaoni wakifanya mambo yanayolifedhehesha Jeshi la Polisi kutokana na ukosefu wa maadili.
Imeandikwa na Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao.