×

Geita Gold Yalamba Fedha za Udhamini Mpya, Yaelekeza Nguvu Kimataifa

Mkataba walioingia Geita Gold FC na GF Trucks utainufaisha klabu hiyo katika mashindano ya kimataifa

KAMPUNI ya uuzaji wa magari makubwa na mitambo GF Trucks imemwaga udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Geita Gold FC.

 

Udhamini huo umesainiwa leo mbele ya Katibu Mkuu wa timu hiyo Simon Shija.

 

Katika makubaliano hayo mbele ya Afisa Biashara Mkuu wa GF Salman Karmali amesema wamefikia hatua hiyo baada ya Geita Gold kufanya vyema katika Ligi Kuu ya NBC.

 

Amesema mbali na kufanya vyema pia kwasasa timu hiyo inawakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa hivyo wameiongezea nguvu ili kupeperusha vyema bendera ya Taifa la Tanzania.

Geita Gold imelamba mkataba huo baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya NBC kwa msimu uliopita wa 2021/2022

” Geita Gold inawakilisha nchi yetu,hivyo tumeona tuwaongezee nguvu ili kuitangaza nchi yetu.” amesema Karmal.

 

Naye Katibu Mkuu Simon Shija amesema wanaishukuru GF Trucks kwa kuwaongezea nguvu na kudai milango ipo wazi kwa makampuni mengine .

 

Geita Gold FC iliyopo chini ya Halmashauri ya Geita imekuwa miongoni mwa timu tishio katika Ligi Kuu NBC.

Leave a Comment