
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilitumia seti ya pili ya fomu za upeperushaji matokeo ambayo ilisuluhisha na vyama vya kisiasa kufunga bahasha zisizoweza kuguswa kabla ya uchaguzi wa Rais wa Agosti 9, 2022, ripoti ya Mahakama imefichua.
Mahakama iliamuru kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo 15 vya kupigia kura kufuatia ombi la wagombeaji wa Azimio la Umoja Raila Odinga na Martha Karua

Timu za kiufundi kutoka kwa Idara ya Mahakama zilipewa jukumu la kuandaa ripoti kuhusu kuhesabiwa upya kura, na uchunguzi wa seva za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)
Vyama vya kisiasa mnamo Julai viliandamana wakati wa uchapishaji wa seti ya pili ya fomu, na kusababisha IEBC kuwaita kwa mkutano wa mashauriano.
Katika mkutano huo, iliamuliwa kuwa seti ya pili ya fomu hazitatumika katika uchaguzi bali zimefungwa katika bahasha zisizoweza kuchezewa.

Katika ripoti yake, timu ya Mahakama inasema ilipata vituo tisa ambako fomu za pili za matokeo zilitumika, baadhi zikiwa na hitilafu katika kujumlisha kura zao.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao