
MAHAKAMA Kuu ya Kenya imetupilia mbali ombi la aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kenya kupitia Azimio la Umoja, Raila Odinga baada ya kujiridhisha kuwa hoja alizowasilisha mahakamani hazikuwa na mashiko.
Odinga aliwasilisha hoja kadhaa mahakamani ikiwemo kuingiliwa kwa mfumo wa kielektroniki wa kuhesbia matokeo ya uchaguzi Kenya, fomu za matokeo kutofautiana na kutofautiana kwa matokeo yaliyotangazwa kwenye vituo nay ale yaliyo kwenye mfumo huo.
Aidha, Odinga alidai kuwa kulikuwa hakuna uwazi katika baadhi ya maeneo wakati wa kuhesabiwa kwa kura hizo, hivyo akaiomba mahakama kufuta matokeo hayo yaliyompa ushindi mpinzani wake, William Ruto.

Katika matokeo hayo Ruto alipata kura 7,176,141 (sawa na asilimia 50.4) na Raila Odinga alipatab kura 6,942,930 (sawa na asilimia 48.85).
Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Juu ya Kenya, likiongozwa na jaji Mkuu wa Kenya, Martha Koome lilipitia hoja zote za upande wa walalamikaji na ushahidi wao pamoja na upande wa walalamikiwa ambao walikuwa Tume ya Uchaguzi ya kenya (IEBC).
Na haya ndiyo yaliyobainika katika kuchambua hoja zote kabla ya kutupilia mbali ombi la Odinga na kumtangaza Ruto kuwa Rais mteule wa kenya.

Jaji Mkuu Martha Koome akisoma maamuzi ya mahakama amesema;
-Tume (IEBC) haikufikia kwa ufasaha usajili wa wapiga kura.
-Tume (IEBC) ilishindwa kudhibiti usalama wa mfumo wake wa kukusanya matokeo.
-Mahakama haijaafiki kuwa kulikuwa na dosari kubwa katika mfumo wa uchaguzi.
-Mahakama yakataa hoja kwamba teknolojia ilishindwa.
Majaji hawakushawishiwa na madai kwamba teknolojia hiyo ilifeli katika majaribio ya uadilifu, uthibitisho, usalama na uwazi, jaji mkuu anasema.
-Hakuna ushahidi kwamba mfumo wa matokeo uliingiliwa
-Majaji wakiangalia suala la kuingiliwa kwa tovuti ya matokeo
-Suala la pili lililoibuliwa na walalamishi ni iwapo kulikuwa na kuingiliwa kwa matokeo kama yalivyopakiwa kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi.
-Hakuna ushahidi kwamba mfumo wa matokeo uliingiliwa
-Jaji mkuu anasema hakukuwa na ushahidi kwamba mtu yeyote alipata mfumo wa utumaji matokeo ili kuvuruga matokeo. Anasema tume ilieleza vya kutosha jinsi mfumo ulivyonasa fomu za matokeo.
-Fomu namba 34A zilizotangazwa na IEBC ni sawa na zile zilizoko mtandaoni.
-Madai kuwa fomu 11,000 za 34A, zilibadilishwa sio kweli.
-Walalamikaji walishindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha.
-Hakukuwa na ushaidi wa fomu namba 34A kutofautiana.
-Ushahidi wa Celestine Opiyo na Arnold Oginga haukuwa wa kweli.
-Ushahidi wa John Githongo haukukidhi kiwango kinachohitajika.
-Mahakama haijashawishika kwamba viwango vya teknolojia ya IEBC vilifeli na kwamba fomu zilizohitajika 32A zilijazwa kwa mafanikio.
-IEBC haikukosea kuahirisha uchaguzi katika maeneo nane na mahakama imejiridhisha kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi huo hakujaathiri matokeo ya kura ya Urais.
-Kura zilizowekwa kimakosa kwenye debe hazikuathiri matokeo ya urais.
-Ujumlishaji wa kura ni jukumu la wafanyakazi wote wa Tume (IEBC).
-Makamishina wanne wa IEBC waliojiondoa na kukataa kuyatambua matokeo yaliyotangazwa na tume hiyo walihusika kuanzia mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi, uchaguzi wenyewe, kuhesabu kura, mpaka mwisho na kujiondoa muda mfupi kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya Urais.
-Makamishina hao hawakuwa na ushaidi wa kutia dosari matokeo ya uchaguzi huo.
-Wafula Chebukati alikosea kujitwika peke yake jukumu lote la matokeo ya uchaguzi na anapaswa kuwa mtumwa wa uamuzi wa Tume.
Baada ya kutoa hoja hizo, Jaji Koome amemtangaza Ruto kuwa rais mteule wa awamu ya tano wa Kenya.