×

Umri ni Namba Tu kwa Wababe Hawa Wawili wa Soka Waliogoma Kustaafu Ulaya

Joaquin Sanchez Rodriguez

JOAQUIN Sanchez Rodriguez mwenye umri wa miaka 41, alizaliwa Julai 21, 1981 huko El Puerto de Santa Maria huko Hispania. Kwasasa anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Real Betis kama winga wa kulia.

 

Alianza safari yake ya soka kama mchezaji wa kulipwa (professional football) katika klabu ya Betis mwaka 2000 baada ya kupandishwa kutoka timu ya vijna ya Betis B na katika misimu hii 7 ndani ya Betis alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 35 katika mechi 256. Mwaka 2006 alijiunga na klabu ya Valencia.

 

Alihudumu katika vilabu vya Valencia,Malaga,Fiorentina na baadae akarudi tena kujiunga na Betis ambapo mpaka sasa anatimiza jumla ya mabao 113 katika mechi 885 alizocheza katika mashindano ya ngazi za vilabu, pia amefunga jumla ya bao 4 katika mechi 51 alizohudumu na timu ya Taifa ya Spain.

Zlatan Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic almaarufu kama Ibra Cadabra mwenye umri wa miaka 40, alizaliwa Oktoba 3,1981 jijini Malmo nchini Sweden. Kwasasa anakipiga katika klabu ya AC Milan kama mshambuliaji huku akivalia jezi namba 11 mgongoni.

 

Alianza mpira katika klabu ya Malmo FF 1999-2001 akipandishwa kutoka timu ya vijana ya Malmo FF. Akifunga jumla ya mabao 16 katika mechi 40 alizocheza kabla ya kuhama kwenda Ajax mwishoni mwa mwaka 2001.

 

Alihudumu katika vilabu vya Ajax,Juventus,Inter Milan,Barcelona,PSG,Manchester United, LA Galaxy na AC milan.Katika maisha yake ya soka amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 510 katika mechi 862 za ngazi ya vilabu, pia amefunga jumla ya mabao 62 katika mechi 121 alizocheza na timu yake ya taifa.

 

Hata hivyo mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi Duniani anayecheza soka la kulipwa ni Robert Carmona raia wa Urugwai mwenye umri wa miaka 60 ambapo hapo awali rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Kazuyoshi Miura raia wa Japan mwenye umri wa miaka 55 anayechezea klabu ya Suzuka Point Getters.

 

Imeandaliwa na Simon Molanga kwa msaada wa mtandao.

Leave a Comment