
Waziri mkuu mpya nchini uingereza aliongea katika hotuba yake ya mara ya kwanza tangu alipopata wadhifa wa kuwa Waziri mkuu na kuahidi kwamba tatizo la kiuchumi lita teketea.
Liz Truss alisema “Nina imani kuwa kwa pamoja tunaweza kuondokana na tatizo hili, tunaweza kujenga upya uchumi wetu, na tunaweza kuwa Uingereza ya kisasa yenye kipaji ambayo najua tunaweza kuwa,”

Waziri mkuu huyo alisema alikuwa na vipaumbele vyake vitatu ikiwemo kupunguzwa kwa ushuru ili uchumi ukuwe, kutatua huduma ya afya kitaifa ambayo inaendeshwa na serikari na kusaidia kupanda kwa gharama za nishati.
Imeandikwa: leocardia Charles kwamsaada wa mitandao.