×

Exclusive: Ali Kamwe Amjibu Mwinyi Zahera, Ataja Hatma Ya Kocha Nabi Yanga -Video

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amezungumza kuhusu maandalizi yao kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika ambao utachezwa tarehe Novemba 1, 2022 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Amesema kwamba, maandalizi yao kuelekea mchezo huo yanaanza na mechi dhidi ya Simba ambayo itachezwa siku ya Jumapili Oktoba 23, 2022, na hivyo mechi hiyo itawapa kipimo sahihi cha maandalizi yao kuelekea mchezo huo.

Aidha, anasema kwamba katika mchezo huo watatumia kila aina ya mbinu ambazo wamezipanga ili kuona kama zitaleta matunda katika mchezo huo na endapo kama zitaleta matunda, basi ndivyo jinsi watavyoondoka nazo kwenda kumkanda Mwarabu siku ya tarehe 2 Novemba.

Pia amesema taarifa zinazosambaa mitandaoni ni mawazo na mitazamo ya wachambuzi wa soka hapa nchini na siyo msimamo wala mawazo ya uongozi wa klabu hiyo na hivyo basi wao wanamtambua Nabi kama kocha wao na hawana mpango wa kumfukuza kocha huyo.

Leave a Comment