×

Mshukiwa wa Pili wa Mauaji ya Watu 10 Waliochomwa Kisu Canada, Akutwa Amefariki

Washukliwa wa mauaji

MSHUKIWA wa pili wa mauaji ya watu 10 waliochomwa kisu aliyekuwa anatafutwa na Polisi wa Canada, Myles Sanderson amekutwa amefariki dunia katika Jimbo la Saskatchewan.

 

Shirika moja la habari nchini humo limesema kuwa kabla ya mshukiwa kufariki alijisalimisha kwa polisi na akachukuliwa na gari la wagonjwa baada ya polisi kuligonga gari alilokuwa akiendesha.

 

Shirika hilo limebainisha kuwa mshukiwa huyo alifariki kutokana na majeraha ya kujiumiza mwenyewe, muda mfupi baada ya kukamatwa na Polisi.

 

Awali, Polisi wa Canada walisema kuwa Myles Sanderson mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa karibu na Mji wa Rosthern, Saskatchewan uliopo karibu kilomita 100 Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Mshukiwa amefariki mara baada ya kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi

Kaka wa mshukiwa huyo ambaye pia na yeye alidaiwa kuhusika na mauaji hayo, Damien Sanderson, mwenye umri wa miaka 31, alipatikana akiwa amefariki dunia Jumatatu karibu na eneo la mashambulizi.

 

Ripoti inaeleza kuwa mashambulizi yaliyotokea Jumapili yalikuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment