×

Wananchi, Viongozi Waanza Kuaga Mwili wa Malkia Elizabeth II Ukitoka Scotland – Video

Gari maalum lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

SAFARI ya mwisho na ya simanzi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza, inaanza mchana wa leo ambapo jeneza lake linasafirishwa kutoka Balmoral kupelekwa kwenye kasri la kifalme la Holyroodhouse huko Edinburgh.

Maelfu ya watu wanatarajia kupanga mstari kando kando ya barabara wakati mwili huo utakapokuwa unasafirishwa.

Hiyo ni hatua ya kwanza ya safari ya maziko yake yatakayofanyika wiki ijayo jijini London.

Mwili umeondoka Balmoral mchana huu , na utasafirishwa taratibu kwa njia ya barabara kuelekea Edinburgh umbali wa takribani maili 175 sawa na 280km.

Kasri la kifalme la Holyroodhouse huko Edinburgh.

Mchakato huo ni sehemu ya kwanza ya msururu wa matukio ya kuomboleza msiba huo utakaokamilishwa kwa maziko ya kiongozi huyo mnamo tarehe 19 mwezi huu wa Septemba.

 

Jeneza lililobeba mwili wa Malkia limefunikwa bendera maalum ya kifalme ya Scotland na kupambwa juu kwa shada la maua.

 

Gari maalum lililobeba maiti yake liliondoka kwenye kasri la Balmoral na kuelekea mji mkuu wa Scotland saa chache zilizopita.

Kifo cha malkia Elizabeth wa pili kimewaliza watu wengi, kusababisha majonzi na kushuhudiwa salamu za rambi rambi za huzuni zikitolewa na watu mbali mbali sio tu na familia ya malkia huyo bali na hata waingereza wengi kwa ujumla wao na duniani.

 

Malkia huyo wa Uingereza ameongoza taasisi hiyo ya kifalme katika jukwa la dunia kwa miongo saba.

Malkia Elizabeth aliitangazwa malkia baada ya kifo cha baba yake mfalme Goerge wa sita mnamo Februari 6 mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka 25.

Sherehe ya kumtawaza rasmi ilifanyika mwaka uliofuatia.

Elizabeth Alexander, mwenye umri wa miaka 69 ni mwanamama aliyezaliwa siku ambayo Malkia Elizabeth alipotawazwa mwaka 1953 hivi sasa ana umri wa miaka 69 ni miongoni mwa waingereza waliojitokeza katika kijiji cha Ballater kilichoko karibu na makaazi ya Balmoral, kusubiri jeneza la malkia hiyo likipita.

Amesema ni jambo la huzuni kwa mtu yoyote kusema kwaheri na anajihisi kama anamuaga kwa mara ya mwisho mtu wa familia,ni jambo linalompa huzuni kutambua malkia hatokuwa nao tena.

 

Binti wa malkia Elizabeth wa pili, mwanamfalme Anne anaandamana na jeneza hilo ambalo litatembezwa kwa mwendo wa taratibu kutoka kasri lake la Balmoral na kupitia miji midogo midogo na vijiji kadhaa hadi katika mji mkuu wa Scotland, Edinburgh ambako jeneza hilo litawekwa katika eneo maalum kwenye kasri la Holyroodhouse.

 

Safari hiyo ya jeneza la malkia huko Scotland ni moja ya msururu wa matukio ya kuelekea maziko ya malkia huyo mjini London tarehe 19 Septemba itakayotangazwa siku ya mapumziko nchini Uingereza.

Leave a Comment