
MOSES Phiri, ingizo jipya ndani ya Simba SC, ameweka rekodi kwa nyota wote wapya waliosajiliwa msimu huu kwa timu za Ligi Kuu Bara kufunga mechi tatu mfululizo ndani ya ligi hiyo.
Kuna maingizo mapya mengi kwenye ligi ikiwa ni pamoja na Stephane Aziz Ki, Gael Bigirimana, Augustine Okrah, Tape Edhinho na Kipre Junior.
Phiri pekee katupia kwenye mechi zote tatu za ligi ambazo amecheza dhidi ya Geita Gold, Kagera Sugar na KMC, zilizochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mzambia huyo aliyetokea Zanaco ya kwao, ameyeyusha dakika 257 kwenye mechi hizo tatu akiwa na uzi wa Simba SC.
STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA