
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imemtambulisha Kocha mkuu mpya, Yusuf Chipo raia wa Kenya kwa mkataba wa mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Juma Mgunda aliyejiunga na Simba Sc hivi Karibuni.
Kocha huyo amejiunga na Coastal Union akitokea Pamba FC ambapo Kabla ya Hapo alikuwa Kayanza FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Burundi.
