
KOREA KUSINI imerejesha (China) mabaki ya wanajeshi 88 wa China waliouawa wakati wa Vita vya Korea, ikiwa ni hatua ya kwanza kufanywa na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol tangu aingie madarakani mwezi Mei.
Walinzi wa heshima wa Korea Kusini walikabidhi masanduku ya mbao yenye mabaki hayo wakati wa hafla katika uwanja wa ndege wa Incheon karibu na Seoul, ambapo yalipakiwa kwenye ndege ya mizigo ya jeshi la anga la China, video ya moja kwa moja ya tukio hilo ilionyesha.

Mabaki hayo yalipokelewa saa chache baadaye katika mji wa kaskazini-mashariki wa China wa Shenyang katika sherehe za kijeshi zilizohudhuriwa na maveterani wa China wa mzozo huo wa miaka mitatu.