×

Zaidi ya Watu 130 Wafariki Kutokana na Mafuriko Nchini Sudan

Mafuriko nchini Sudan

ZAIDI ya watu 130 wamefariki dunia na wengine kadhaa wamenusurika kifo kwa sababu ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko nchini Sudan.

 

Mafuriko hayo yamesababisha uharibu mkubwa katika makazi ya watu ambapo inakadiria kuwa zaidi ya nyumba 128,000 zimeharika na kwamba tayari serikali imetangaza hali ya dharura katika majimbo 18 ya nchi hiyo.

 

Mafuriko yamesababisha uharibifu wa miundombinu nchini humo

Ripoti inaeleza kumekuwa na ongezeko la vifo vya watu kutoka 112 hadi 134 ndani ya mwezi huu huku Jimbo la Kordofan lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo likiongoza kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, majimbo mengine yaliyoathiriwa na mafuriko hayo ni Gedaref, Kassala na Darfur.

Vikosi vya ukoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji

Shirika hilo linahofia kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka huu huenda watu 460,000 wakaathiriwa na mafuriko hayo nchini Sudan.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment