
MTU mmoja ambaye jina lake halijawekwa wazi amewekwa chini ya ulinzi baada ya kulisogelea jeneza la Malkia Elizabeth ambapo alitoka kwenye mstari maalum na kusababisha taharuki katika eneo hilo.
Taarifa kutoka Bungeni zimebainisha kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa majira ya saa nne usiku ambapo hadi sasa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi ambapo Metropolitan Polisi wamethibitisha kumshikilia mtu huyo.

Msemaji wa Bunge alithibitisha kutokea kwa tukio hilo:
“Tunajua kilichotokea katika ukumbi wa Westminster, ambapo mtu mmoja alitoka kwenye mstari na kulisogelea jeneza la Malkia Elizabeth II, tayari watu wameondolewa katika ukumbi na zoezi la kutoa heshima za mwisho limeanza upya kwa uangalifu mkubwa.”
Mwili wa Malkia Elizabeth II unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu ya wiki ijayo