
ZAIDI ya wanamgambo 100 wa al-Shabab wameuawa katika operesheni katika muda wa siku tatu zilizopita na Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA), ambalo linapokea msaada kutoka kwa vikosi vya Amerika, katika eneo la kati la Hiiraan, serikali ilisema Jumatatu.
Hiiraan na eneo jirani la Galgudud limekuwa kitovu cha makabiliano ya wiki kadhaa kati ya wanamgambo wa koo wanaoungwa mkono na serikali na wapiganaji wa al-Shabab.

Televisheni ya taifa siku ya Jumatatu pia iliripoti kuwa jeshi limewaua wanamgambo wasiopungua 54 katika mkoa wa Hiiraan.
Siku moja kabla, jeshi lilisema zaidi ya wanamgambo 75 waliuawa katika operesheni ya pamoja na wanamgambo wa koo.
Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao