×

Programu ya Kampeni za Hillary Clinton Yadukuliwa

CEDAR FALLS, IA - MAY 19: Democratic presidential hopeful and former Secretary of State Hillary Clinton hosts a small business forum with members of the business and lending communities at Bike Tech bicycle shop on May 19, 2015 in Cedar Falls, Iowa. Yesterday Clinton hosted an organizing rally with supporters in Mason City. (Photo by Scott Olson/Getty Images)Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.

Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.

Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.

Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.

Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

Leave a Comment