×

Ni Kidijitali Zaidi kwa Wateja wa Benki ya Azania, Yaja na Sapraiz Kwa Wateja Wake

Meneja wa Huduma za Benki Kidijitali wa Benki ya Azania, Bw. Vinesh Davda akiwaelekeza wanahabari (hawapo pichani) jinsi mfumo huo unavyofanyakazi.

 

 

BENKI ya Azania inayomilikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii imezindua huduma ya Azania Tap & Go ikiwa ni muendelezo wa kuboresha huduma za benki hiyo zinazotolewa kidijitali. Kwa miaka kadhaa benki ya Azania imechukua hatua kubwa kuhakikisha inakua na kuboresha huduma zake kwa Watanzania.

Meneja wa Huduma za Benki Kidijitali wa Benki ya Azania, Bw. Vinesh Davda (katikati) walivyozindua huduma hiyo, kulia ni Meneja Masoko wa Benki hiyo Allan Msalilwa na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa benki hiyo, Halima Sembunge.

 

Azania Tap & Go ni huduma ambayo inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa urahisi kwa kugusisha tu kadi yake ya Visa UnionPay, Mastercard au Umoja katika mashine ya kufanyia malipo (PoS) ambazo zimesambazwa na benki hiyo sehemu mbalimbali za kutolea huduma kama vile maduka makubwa, hotel na sehemu za starehe, hospitali vituo vya kuuza mafuta n.k.

Sehemu ya mashuhuda waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio.

 

 

Kupitia huduma hii mmiliki wa kadi sasa hatakuwa na haja ya kubeba pesa taslim. Lakini pi huduma hii itawawezesha wafanyabishara na wamiliki wa sehemu za biashara kuepuka kupokea pesa taslimu badala yake malipo yatakwenda moja kwa moja benki hivyo kumhakikishia mfanyabiashara usalama wa pesa zake.

 

Akiongea katika uzinduzi huo meneja wa huduma za Benki Kidijitali wa Benki hiyo, Bw. Vinesh Davda alisema kuwa kwa kutumia kadi za Visa, UnionPay , Mastercard au Umoja kupitia huduma ya Tap and Go sasa wateja wa benki yoyote wanaotumia kadi hizo wataweza kufanya manunuzi kisha kufanya malipo kwa urahisi kwa kutumia kadi zao kwenye maduka mbalimbali na kadhalika ambayo yatawekewa mashine ya kufanya malipo hayo kwa kadi inayoitwa PoS machine.

 

“Katika kuendelea kuwajali wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwa kutuunga mkono kwa miaka 27 tumehakikisha wanaendelea kufurahia huduma zetu zote zikiwamo za kibenki kidijitali, kwa kutumia kadi zao” aliongeza Bw. Davda.

 

Benki yetu imewekeza katika teknolojia ya kisasa, mfumo wetu wa teknolojia ya kibenki ni wa kisasa zaidi na ndio uliotuwezesha kutuunganisha na huduma hii kirahisi na wanaomiliki kadi za benki sasa wataweza kufanya malipo kwa kutumia kadi zao kwa kugusisha tu kadi yako kwenye mashine hiyo ya PoS na tayari muamala utakuwa umekamilika”. Meneja huyo alimalizia kwa kusema kuwa huduma hii itawapa urahisi zaidi watumiaji.

 

“Ukiwa na kadi ya Visa, UnionPay au Mastercard kupitia mashine hii ya PoS ya Azania muamala unakamilika kwa kugusisha tu kadi yako juu ya mashine hii lakini pia hata wale wenye kadi za Umoja pia watakamilisha muamala kwa kuchomeka tu kadi hiyo kwenye mashine ya PoS na kisha kuichomoa.”

 

Alimaliza kusema Bw. Davda huku akiwasihi Watanzania kutumia mashine ya PoS ya Benki ya Azania kwani ni rahisi kutumia na inapokea kadi za aina zaidi ya moja.

 

Ili kupata maelezo zaidi juu ya huduma za Benki ya Azania tembelea tawi lolote la benki hiyo hapa nchini au tembelea tovuti ya www.azaniabank.co.tz au piga simu 0800110210 ni bure.

Leave a Comment