×

NMB Yashinda Tena Tuzo Ya Benki Bora Wateja Binafsi

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Serikali wa Benki ya NMB, Amanda Feruzi (kulia) na Meneja Mwandamizi wa Mahusianao ya Biashara ya Nje ya Nchi wa Benki ya NMB, Lucy Kimei (kushoto) wakifurahia tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara Tanzania kwa mwaka 2022 kutoka jarida la Global Banking and Finance Mara baada ya Hafla ya Ugawaji Tuzo uliofanyika jijini London nchini Uingereza hivi karibuni.

 

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Benki ya NMB imeshinda tuzo ya benki kiongozi wa kuwahudumia wateja binafsi nchini kutokana na ubora wa huduma zake kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha za umma wa walio wengi.

 

NMB ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora ya Wateja Binafsi Tanzania kwa mwaka 2022 kwenye hafla ya tuzo za Global Banking and Finance (GBAF) Awards zilizofanyika huko London, Uingereza.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2011 na jarida la Global Banking & Finance Review lenye wasomaji zaidi ya milioni tatu ulimwenguni kote na ambalo shughuli yake kubwa ni kuangazia matukio na maendeleo ya kifedha duniani.

 

Leave a Comment