
Miongoni mwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema waliojitosa kuwania nafasi ya ujumbe mkutano mkuu CCM Taifa ni Dr Omari Sukari ambaye ni Mganga mkuu wa mkoa wa Katavi
Akizungumuza na katika ofisi za CCM wilayani hapo Dkt. Sukari amesema aliamua kuwania nafasi hiyo ili akitumike chama chama cha mapinduzi.
Amesema nafasi ya ujumbe wa mkutano mkutano mkuu Taifa siyo kazi ndogo vikao vya halmashauri kuu vilika na kupitisha jina lake kuwa miongoni mwa watakao wania nafasi hiyo.
“Nitajitoa kwa hali na mali kuwatumika wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi katika nafasi ili tuisadie serikali” amesema Sukari.
Mmoja wa wanaCCM John Amos amesema kuteuliwa kwa watumishi wa serikali kuwania nafasi za uongozi ndani ya CCM kumeonyesha jinsi chama kilivyokomaa katika siasa ndani na nje ya chama.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Muhusin Zikatimu amesema majira ya wanaCCM wote walioteuliwa kuwani nafasi mbalimbali ndani ya chama wanasifa hivyo CCM ijiandae kupata viongozi bora.
Kundi kubwa la wafanyakazi wa Serikali ni miongoni mwa wanaCCM walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi