Kampuni ya Wentworth Gas Ltd Yawekeza Katika Jamii
KAMA sehemu ya mpango wa kuwekeza katika jamii Kampuni ya Wentwoth Gas Ltd ilikuwa kati ya wadhamini wa mashindano ya Dar Touch Rugby Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Timu ya Arusha Rhinos waliibuka washindi wa Dar Touch Rugby Tournament -2022 kati ya timu zaidi ya 20 zilizoshiriki.