
Mwamuzi wa kati, Hans Mabena kutoka mkoani Tanga aliyechezesha mchezo wa Ligi kuu ya NBC kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Azam FC amepelekwa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu jambo lililosababisha ashindwe kumudu mchezo huo
Tanzania Prisons ilishinda 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Septemba 30, 2022.
Afisa Habari wa klabu ya Azam FC Thabiti Zakaria maarufu ZakaZakazi amefungiwa miezi mitatu na kupigwa faini ya Shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kuwatuhumu marefa kuwanyima penati mbili kwenye mchezo Azam FC waliocheza na Tanzania Prisons.

