×

Rais Museveni Aiomba Msamaha Kenya na Afrika Mashariki Kwa Niaba ya Mwanaye

Jenerali Muhoozi Kainerugaba

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewaomba radhi wananchi wa Kenya na Wana-Afrika Mashariki kwa ujumla kufuatia mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuandika kwenye mtandao Twitter kauli ambazo zililenga kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia ikiwemo kauli ya kutaka kuiteka Nairobi na kumtaka Uhuru Kenyatta agombee muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

 

Rais Museveni amesema haikuwa sahihi kwa Muhoozi ambaye alikuwa Mkuu wa Jeshi la Ardhini la Uganda kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo jana, kuandika alichokiandika na kusema ule haukuwa msimamo wa Serikali ya Uganda.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa Rais wa sasa wa Uganda Yoweri Museveni alitishia kuivamia Kenya

Museveni ametolea ufafanuzi pia sababu za kumpandisha cheo Muhoozi kutoka Luteni Jenerali na kumpa cheo cha Ujenerali licha ya kauli zake hizo tata ambapo amesema pamoja na kosa hilo, lakini Muhoozi anayo mazuri mengi na mchango mkubwa alioutoa na anaoweza kuendelea kuutoa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

“Nimetumia utaratibu wa kuoneshwa kutopendezwa na mabaya huku wakati huohuo nikimtia moyo Muhoozi kwa mazuri yake.

 

“Samahani sana ndugu zetu Wakenya na eatu wa Uganda ambao mlikwazwa na kauli za Muhoozi, mbali na ombi hili la wazi nimewasilisha pia samahani yangu nyingine ya siri kwa Rais wa Kenya, William Rutto.”

Leave a Comment