×

Watu 76 Wafariki Dunia Katika Ajali ya Boti Nchini Nigeria

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

WATU 76 wameuawa kati ya 85 waliokuwepo kwenye Boti iliyopata ajali nchini Nigeria na kwamba taarifa hiyo imethibitishwa na wafanyakazi wa huduma za uokoaji wa dharura.

 

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kuwa karibu wasafiri wote waliokuwepo katika boti iliyopinduka kwenye mto Niger wamefariki dunia.

 

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Rais, Muhammadu Buhari imemnukuu kiongozi huyo akiwaombea dua watu waliopoteza maisha na kuzitakia afueni familia zilizopoteza wapendwa wao na kusisitiza idara zinazohusika kuzifariji familia hizo.

Boti imezama na kusababisha vifo vya watu 76

Mratibu wa huduma za dharura ngazi ya taifa Kusini mwa Nigeria, Thickman Tanimu amesema kuongezeka sana kwa kina cha maji ya mto Niger katika eneo la Ogbaru kumesababisha kukwama kwa shughuli za uokoaji.

 

Ajali za majini hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, kutokana na vyombo kupakia abiria wengi kuliko uwezo wake, kasi kubwa, uchakavu wa vyombo hivyo na kutojali kanuni za usafiri wa majini.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave a Comment