
RAIS wa Marekani Joe Biden amesema kuwa Vladimir Putin ni mtu mwenye busara ambaye amehukumu vibaya matarajio yake ya kuichukua Ukraine.
” Nadhani ni mtu mwenye busara aliyefanya mahesabu vibaya.”
Kwa mujibu wa Biden ni kuwa Putin alihisi itakuwa ni rahisi kuivamia Ukraine na alihisi watu wa Ukraine watamkaribisha kwa mikono wazi sababu pale ni nyumbani kwa Urusi ila Vladmir alikuwa amekosea kufikiria hivyo aidha wanajeshi wa Urusi wote kiujumla wamedharau ukali na ukaidi wa Ukraine.
Biden anaamini kuwa Putin ni mtu mwenye busara na kuwa hawezi kufikia maamuzi ya kutaka kutumia mabomu ya nyuklia kwa kupambana na Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, ambaye ni Raisi wa Ukraine aliishtaki nchi ya Urusi kwa kufanya mavamizi ya kigaidi dhidi ya daraja la Crimea’s Kerch ambapo bomu lilifyatuliwa.
Rais Zelensky amesema siku ya jumanne kuwa kati ya makombora 28 yaliyorushwa na nchi ya Urusi yaliyofanikiwa kuzuiwa ni 20 ikiwemo na ndege ndogo zisizo na rubani (drones).
Katika pambano hilo Ukraine walifanikisha kuharibu vifaa vya Russia na bohari lake la silaha na kupelekea vifo vya wanajeshi wa Urusi ishirini na tatu.

Viongozi wa G7 ambao wanaipatia Ukraine msaada wa mifumo ya kujihami wamesema kuwa wataendelea kuwa bega kwa bega na Ukraine, hivi karibuni Zelenskiy aliwaomba viongozi wa G7 kumpatia mifumo ya ulinzi na tume ya ufuatiliaji kwenye mipaka ya Belarus.
Majeshi ya Kyiv yamekuwa yakiwadhibiti askari wa Urusi kwenye mstari wa mbele huko kusini na mashariki, ambapo Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky amesema wamefanikiwa kuteka eneo lenye kilomita ya mraba 2,500.
Wajerumani wameahidi kuipatia nchi ya Ukraine makombora yaitwayo Iris-T ili yatumike kama ngao kwa kulinda mji wa Ukraine.
Wiki iliyopita Rais Joe Biden alionya hatari ya matumizi ya nyuklia itakayo pelekea mwisho wa dunia kuwa vitisho vinavyotolewa na nchi ya Urusi vinaweza pelekea majanga kama vile kufanya makosa na mahesabu mabovu, ingawa Biden hakutoa jibu kuhusiana na nchi ya Marekani itafanya nini ikitokea Urusi kutumia kifaa cha nyuklia kwenye uwanja wa vita dhidi ya Ukraine.
Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao