×

Mwandishi wa Habari wa Pakistan Auawa kwa Kupigwa Risasi

Mwandishi wa Habari wa Pakistani, Arshad Sharif

MWANDISHI wa Habari wa Pakistan, Arshad Sharif ameuawa usiku wa Jumapili katika Jimbo la Kajiado lililopo katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi.

 

Polisi wa Kenya wamethibitisha taarifa hiyo na kueleza kuwa Msemaji wa Polisi, Bruno Shioso anachunguza chanzo kilichosababisha kifo cha Sharif.

 

Vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo vimesema mwandishi huyo alipigwa risasi kwenye kizuizi cha barabara kuu ya Nairobi kuelekea Magadi.

Msemaji wa Polisi Nchini Kenya, Bruno Shioso

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, mke wa mwandishi huyo, Jeveria Siddique alisema kuwa siku ya Jumatatu amempoteza rafiki, mume na mwandishi wa habari anayempenda.

 

Rais wa Pakistan, Arif Alvi amesema kifo cha Arshad Sharif ni pigo kubwa kwa waandishi wa habari na Pakistan na kuiitaka familia ya Sharif kuwa wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu, Innalillahi Wainnalillah Rajuuni.

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa Msaada wa Mtandao

Leave a Comment