
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Omary Sukari amesema atatumia nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu taifa kupitia dhamana aliyopewa na chama chake kuwaunganisha na kuwa kitu kimoja lengo ni kuimalisha chama.
Amesema CCM nichama kilichona misingi ya kweli na imara hivyo misingi hiyo inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa kama ilivyoasisiwa na viongozi wa ngazi za juu.
Sukari amefafanua kuwa wabunge wa majimbo ya Sengerema na Buchosa wanafanya kazi nzuri za kutekeleza Ilani ya CCM hivyo wanatakiwa kutiwa moyo na kuunga mkono kazi wanazofanya ili wananchi wapate maendeleo.
“Sisi kama viongozi wa chama tuliochaguliwa na kupewa dhamana hii kubwa nikuhakisha chama kinaendelea kushika hatamu na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo, amesema Sukari.
Katika nafasi nyeti ya uwakilishi wa mjumbe mkutano mkuu Taifa Dkt. Omari Sukari alichaguliwa na wajumbe kwa kura akifuatia na Joshua Shimiyu alipata kura 720 sambamba na Jackilin George alipata kura 571 wote walichaguliwa kwenye nafasi hiyo.
” Mmetupa heshima sisi mkatuona bora kuliko wengine, sisi ni sura mpya tutawatumikia bila woga na tumekubali kutumwa ,amesema Sukari.
Joshua Shimiyu mjumbe wa mkutano mkuu Taifa amesema licha ya kugombea ubunge ndani ya CCM kwa miaka kadhaa na kushindwa lakini akapata nafasi ya uwakilishi ndani ya CCM wamenmpatia heshima kubwa ambayo ataiwatumikia kwa moyo mmoja kwa nafasi hiyo.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya Wilaya ya Sengerema Muhusin Zikatimu amesema yeye kama mtendaji mkuu wa chama atahakikisha anatoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi wote waliochaguliwa ili chama kiweze kusomga mbele.
Mmoja wa wana CCM wilayani humo, Jonathani Amos amesema misingi ya CCM ya umoja ushirikiano na ushindi inatakiwa kufuatwa ili CCM iendelee kuwa madarakani.