ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Nitashukuru ila na wewe jiandae kwa sapraizi zangu vilevile,” John alimwambia Madam Martha.“Sapraizi gani?” Madam Martha alimwuliza.SASA SONGA MBELE…
John alipoulizwa hivyo, alicheka na kumwambia asiwe na haraka asubiri kuziona kadiri penzi lao litakavyozidi kuishi.“Wewe John una maneno sana, eti kadiri penze letu litakavyozidi kuishi, kwani wewe ulifikiria litakufa?” Madam Martha alimwuliza.
“Kwa jinsi tulivyo na tofauti na kwa kuwa tayari kuna mtu wa tatu kaujua uhusiano wetu, halitakuwa na maisha marefu ,” John alimwambia mwalimu wake.
“Tofauti iliyopo kati yangu na wewe ni ipi, mimi si mwanamke kama wengine?” Madam Martha alimwuliza John.
John alimwambia mwalimu wake huyo kwamba, kwanza walikuwa na tofauti kubwa ya umri, pili alikuwa mwalimu wake na tatu tayari mwalimu Anna alijua wao ni wapenzi.
“John mpenzi wangu, ondoa wasiwasi kuhusu umri, elewa kwamba mapenzi ni sawa nyuki asiye chagua ua la kutua, kuhusu mwalimu Anna hana tatizo,” Madam Martha alimwambia.
Licha ya Madam Martha kumtoa wasiwasi, John alikuwa na hofu kuendelea kuwa na uhusiano na mwalimu wake akamweleza alihofia kama siri hiyo ingetoka angefukuzwa shuleni na sijui angemwambia nini baba yake hadi amwelewe.
“John!” Madam Martha alimwita.
“Nakusikia madam!” aliitika.
Alipoitika, mwalimu huyo alimwambia miongoni mwa wanafunzi wenye bahati yeye alikuwa miongoni mwao kwani alitokea kupendwa na mwalimu wake.
“John huoni kama hiyo ni bahati ya pekee?” Madam Martha ambaye hakuwa tayari kuona anampoteza John kirahisi alimwambia.
Hakuishia hapo, alimwambia kwamba hakuna mtu atakayebaini kama walikuwa wakitoka kimapenzi zaidi ya mwalimu Anna aliyemuweka sawa.
Baada ya John kuhakikishiwa hivyo alifurahi, kwa kuwa alikwishampa mambo matamu alimuomba Madam Martha amruhusu aondoke.
“Hakuna shida, ila naomba uhusiano wetu uwe siri usimwambie rafiki yako yeyote, sawa mpenzi wangu?” Madam Martha alimwambia John.
“Sitathubutu kufanya hivyo kwani hatari ya jambo hilo naielewa,” John alimwambia Madam Martha.
Kwa kuwa nyumba hiyo ya mwalimu ilikuwa na bafu uani, Madam Martha aliandaa maji ya kuoga lakini alipomwambia John wakaoge wote, kwa uoga aliokuwanao kijana huyo alikataa.
Madam Martha hakuona sababu ya kumlazimisha kwani alijua kadiri siku zitakavyokwenda mbele na penzi lao kukolea kuoga pamoja litakuwa jambo la kawaida.
John alipomaliza kuoga, akiwa kajifunga taulo kama vile alikuwa baba mwenye nyumba, alirudi ndani ambako alivaa nguo lakini kabla ya kuaga, Madam Martha alichukua pochi yake ndogo iliyokuwa juu ya kabati la kujipambia.
Akiwa ameishika pochi hiyo, aliifungua na kuchomoa noti ya shilingi elfu kumi akampatia John na kumwambia akanunue chochote alichohitaji.
“Asante madam!” John alishukuru.
“Usiniite madam, niite mpenzi,” Madam Martha alimwambia John aliyeishia kucheka.
“Basi kuanzia kesho nitakuwa nakuita mpenzi,” John alimwambia.
Mtu na mwalimu wake hao baada ya kutaniana hapa na pale, John aliondoka na kuelekea kwao akiwa mwepesi baada ya kumpa usumbufu wa raha mwalimu wake.
“Mambo si ndiyo haya, penzi tamu la madam nimelifaidi na teni juu au ndiyo sapraizi alizoniahidi nini?” John alijisemea moyoni huku akielekea kwao.
Alipofika nyumbani alimkuta baba yake akiwa sebuleni anasoma gazeti la Uwazi akamsalimia kisha akazama chumbani kwake, akajilaza kitandani na kuanza kutafakari mambo waliyoyafanya na mwalimu wake.
“John, huoni kama una bahati ya kupendwa na mwalimu wako?” John alirudia kuitafakari kauli iliyotolewa na Madam Martha.
Kijana huyo mtanashati hakuishia hapo alifikiria mambo mengi ikiwa ni pamoja na tukio la kukutwa na mwalimu Anna akiwa kitandani na Madam Martha.
Baada ya kutafakari kwa muda alitoka chumbani na kuendelea na mambo mengine, kesho yake kama kawaida aliamka asubuhi na mapema akajiandaa na kwenda shuleni.
Alipofika alishangaa kuona walimu na wanafunzi wakiwa wamesimama kwa makundi.
Kwa kuwa haikuwa kawaida akahisi kulikuwa na tatizo kubwa, kama hapakutokea uizi basi kulikuwa na msiba.
Mwananfunzi wa kwanza kukutana naye alikuwa Patrick ambaye alimsalimia na kuhoji kuhusiana na hali ya utulivu iliyokuwa pale shuleni.
“Kwani huna habari ya msiba?” Patrick alimwuliza John.
“Msiba wa nani?” John alimwuliza kwa hamaki.
Patrick alimfahamisha kwamba Madam Martha alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia siku hiyo.
“Unasemaje Patrick?” John ambaye hakuamini alichokisikia alimwuliza Patrick.
“Ndiyo hivyo tumepata pigo kubwa sana la kuondokewa na Madam Martha ambaye alikuwa mwalimu mzuri na aliyependa kucheka na kila mtu.
Wakati John na Patrick wanazungumza, mara walimu na wanafunzi wakaanza kulia, shule nzima ikatawaliwa na vilio.
John alishindwa kujizuia kulia ambapo alisema; “Umeondoka mwalimu wetu Madam Martha, tutakuwa tukitaniana na nani, nani atakuwa akitufundisha somo la sayansi kama wewe?”
Licha ya wanafunzi wa kiume kulia sana lakini John alifanya hivyo mara dufu hadi alipofuatwa na mwalimu Anna aliyejua kilichojificha nyuma ya pazia baina ya Madam Martha na John na kumbembeleza anyamaze, John akaacha kulia.
Taratibu za kusafirisha mwili wa Madam Martha kwenda kwao kwa mazishi zilipokamilika, wakati wa zoezi la kuuaga mwili wake John na wanafunzi wengine walilia sana na kusema; “ooh…Madam Martha” ukalale pema peponi. Mwisho.
Kama una maoni, ushauri kuhusiana na chombezo hili tumia namba hiyo hapo juu.
Mmmh…Mbona mapema ivo?
Chombezo lilikuwa limeanza kunoga ilo.
Kwa Kweli hapo umepunguza Uhalisia.
nataman kujua kinachorndelea