Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea maeneo ambayo bado hayajakamilika wakati alipokagua ujenzi wa Kituo cha Afya Matanga kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga ambacho kimeanza kutumika ingawa ujenzi wake bado haujakamilika katika baadhi ya maeneo ambapo amebaini baadhi ya mapungufu na kutoa mwongozo wa kutekeleza.