The House of Favourite Newspapers

Washindi 24 wa Kampeni ya Wakishua Wajizolea Milioni Kila Mmoja, 6 Vifaa Vya Hisense

0
Meneja wa Wateja Maalu wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

Dar Salaam 16 Desemba 2022:  Wakati kampeni ya Wakishua inayoendeshwa na Kampuni mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kupitia huduma ya Tigo Pesa kwa kushirikiana na kampuni ya vifaa vya nyumbani vya kisasa ya Hisense ikiendelea leo washindi 24 wamekabidhiwa pesa taslimu shilingi milioni moja na wengine sita wameibuka na vifaa vya Hisense.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;

Afisa Masoko wa Hisense, Joseph Mavula akizungumza baada ya kuwakabidhi vifaa vya Hisense washindi.

 

“Leo tuna tukio la kukabidhi zawadi kwa washindi wetu ambapo mpaka sasa tumeshafanya droo tatu na tumeshapata washindi 24 waliojishindia  pesa taslimu shilingi milioni moja kila mmoja na washindi wengine sita waliojishindia vifaa vya nyumbani vya Hisense.

“Vifaa hivyo vya kisasa kabisa kutoka Hisense ni microwave, spika muziki, friji na Tv ya nchi 55”. Alisema meneja huyo.

Mshindi wa milioni moja akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa.

 

Aliendelea kusema kuwa wanawasihi wateja wao kufanya miamala kwa maana kuna droo nyingi zaidi zinaendelea kufanyika mpaka Januari 18 mwakani hivyo huwezi jua huenda ukaibuka mshindi kwenye droo ya milioni moja kila wiki au vifaa vya Hisense.

Meneja huyo amesema kuwa mwishoni mwa kampeni hii ukajishindia pesa taslimu shilingi milioni 10, milioni 20 au ndinga la kishua aina ya Toyota Rush ambayo haijawai kutumika 0km.

Mmoja wa washindi wa vifaa vya Hisense akisimamia vifaa vyake vilipokuwa vikiingizwa kwenye usafiri aliokwenda nao.

 

“Hivyo nawasihi kufanya miamala ya Tigo Pesa kulipa bili, kutuma na kupokea pesa, kupokea pesa kutoka benki au mitandao mingine au nchi za nje ili uweze kuingia kwenye droo na kuweza kujishindia zawadi hizo”. Alimaliza kusema meneja huyo.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Hisense alisema;

“Leo tunatoa zawadi kwa washindi wa droo ya pili nay a tatu wa kampeni hii ya Ndinga la Kishua, mamilioni ya pesa na vifaa vya Hisense.

“Mpaka siku ya leo tumeshapata washindi sita wa vifaa vya Hisense ambavyo ni Tv nchi 50, sound bar, microwave pamoja na friji.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwahamasisha Watanzania wote kufanya miamala ya Tigo Pesa kwa ili kujiongezea nafasi yakuingia kuingia kwenye droo ya kampeni hii ya kujishindia mamilioni ya pesa, vifaa vya Hisense na ndinga la kishua.

“Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwahamsisha Watanzania kufika katika maduka yetu ya Hisense kujipatia vifaa Hisense ili waweze kujipatia vifaa vya Hisense kwa punguzo mpaka la asilimia 20 katika kipindi hiki cha sikukuu”. Alimaliza kusema afisa masoko huyo.

Leave A Reply