
KIUNGO Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye hivi karibuni aliaga ndani ya kikosi cha Yanga alichokitumikia kwa miaka minne, ameondoka nchini na kutimkia Dubai kwa mapumziko.
Nyota huyo ambaye amekuwa akihusishwa kutakiwa na Azam FC baada ya kuaga Yanga, Alhamisi ya wiki hii alionekana kwenye Uwanja wa Mao Zedong uliopo Unguja, Zanzibar akicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege huku yeye akiitumikia JKU, timu ambayo ilimtoa kabla ya kutua Yanga.

Mapema jana, Fei Toto aliweka picha na video kwenye akaunti yake ya Instagram ikimuonesha yupo kwenye ndege, kisha akaandika: “Alhamdulillah nimefika salama tayari kwa kuanza majukumu yangu Mapya.”
Mtu wa karibu na nyota huyo, ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Fei Toto ameelekea Dubai kwa mapumziko kidogo.”
Fei Toto ambaye hadi anaondoka Yanga alikuwa nyota muhimu kikosini hapo akiwa nahodha msaidizi, ambapo amefunga mabao sita katika Ligi Kuu Bara msimu huu.
STORI NA MWANDISHI WETU, SPOTI XTRA