
Watu 18 wameuawa akiwemo waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine baada ya helikopta kuanguka kando ya shule ya chekechea katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Kyiv.
Watoto watatu walikuwa miongoni mwa waliofariki na wengine 15 walikuwa wakitibiwa hospitalini.
Waziri, Denys Monastyrskiy, alikuwa na watu wengine wanane kwenye helikopta hiyo.
Naibu waziri wake wa kwanza na katibu wa serikali pia walikufa, maafisa walisema, wakati helikopta hiyo iliposhuka katika kitongoji cha Brovary.
Mabaki ya helikopta yalikuwa nje ya jengo linalowaka moto.
Moto ulizuka karibu na shule ya chekechea na watoto na wafanyikazi walihamishwa kutoka kwa jengo hilo.
Kulikuwa na giza na ukungu wakati wa ajali hiyo na ripoti za awali zinasema helikopta hiyo iligonga shule ya chekechea kabla ya kuanguka karibu na jengo la makazi.