The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Marekani lamua Kiongozi wa Islamic State (ISIS) nchini Somalia

0

US MILITARY OPERATION-SOMALIA Jeshi la Marekani liliendesha operesheni ambayo ilimua afisa kiongozi wa kundi la Islamic State kaskazini mwa Somalia, maafisa wa Marekani wamesema Alhamisi.

Maafisa hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wamewambia waandishi wa habari kwamba Bilal al-Sudani, aliyetajwa na Marekani kama kiongozi wa ISIS nchini Somalia, aliuawa katika operesheni pamoja na washirika wake 10.

Wameongeza kuwa operesheni hiyo iliidhinishwa na Rais Joe Biden mapema wiki hii na kuendeshwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Maafisa hao walikataa kujadili maelezo ya msingi kuhusu operesheni hiyo. Walikataa kueleza tishio lolote la moja kwa moja lililosababishwa na Sudani kwa Marekani, kutoa maelezo ikiwa taarifa zozote za kijasusi zilikusanywa, jinsi jeshi la Marekani lilivyoendesha operesheni hiyo au ni wanajeshi wangapi walihusika katika operesheni hiyo.

TUNDU LISSU ALIPUA TENA, SERIKALI YAJIBU MAPIGO, MAZITO PANGA la RAIS SAMIA | FRONT PAGE

Leave A Reply