×

Maelfu Wataka Kumuasili Mtoto Mchanga Aliyezaliwa chini ya Vifusi vya Tetemeko la Ardhi Uturuki

Maelfu ya watu wamejitokeza kutaka kumuasili mtoto wa kike aliyezaliwa chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka kaskazini-magharibi mwa Syria, kufuatia tetemeko la ardhi la Jumatatu.

Alipookolewa, mtoto huyo aliyepewa jina la Aya – maana yake muujiza kwa Kiarabu – alikuwa bado kitovu chake kilikuwa kimeungana na mamake aliyejifungua kwenye kifusi. Mama yake, baba yake na ndugu zake wote wanne walifariki baada ya tetemeko hilo kupiga mji wa Jindayris.

Aya sasa yuko hospitali. “Alifika Jumatatu akiwa katika hali mbaya sana, alikuwa na michubuko, alishikwa na baridi na alikuwa anapumua kwa shida,” alisema Hani Marouf, daktari wa watoto anayemuhudumia.

Sasa yuko katika hali thabiti. Video za uokoaji wa Aya zilienea kwenye mitandao ya kijamii. Picha zilionyesha mwanamume mmoja akikimbia kutoka kwa kifusi cha jengo lililoporomoka, akiwa amemshikilia mtoto mchanga aliyekuwa ameenea vumbi.

Khalil al-Suwadi, jamaa wa mbali, ambaye alikuwepo wakati alipookolewa, alimleta mtoto mchanga huyo kwa Dk Marouf katika jiji la Syria la Afrin.

Maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii sasa wamekuwa wakiomba maelezo ya namna ya kumuasili. “Ningependa kumchukua na kumpa maisha ya heshima,” alisema mtu mmoja.

Mtangazaji wa televisheni ya Kuwait alisema, “Niko tayari kumtunza na kumlea mtoto huyu… ikiwa taratibu za kisheria zitaniruhusu.”

Meneja wa hospitali anakohudumiwa mtoto huyo, Khalid Attiah, anasema amepokea simu nyingi kutoka kwa watu kote ulimwenguni wakitaka kumuasili mtoto Aya.

Dk Attiah anayemuhudumia na ambaye ana binti mchanga wa tofauti ya minne zaidi, alisema, “Sitaruhusu mtu yeyote kumlea kwa sasa hadi itakapopatikana familia yake, ninamchukulia kama mmoja wa watoto wangu.”

Kwa sasa, mkewe na Dk Attiah ndiye anayemnyonyesha pamoja na binti yao wenyewe.

Katika mji wa nyumbani kwa Aya wa Jindayris, watu wamekuwa wakitafuta wapendwa wao katika majengo yaliyoporomoka.

MASTAA YANGA WAWEKEWA BILIONI 1.6 KUMUUA MWARABU, SIMBA MIKAKATI MIZITO CAF | KROSI DONGO

Leave a Comment