
Mwanadada Robyn Fenty ‘Rihanna’ ameweka wazi kuwa ana ujauzito wa mtoto wa pili na mpenzi wake ambaye pia ni msanii mwenzake, Asap Rocky.
Rihanna ameyasema hayo jana Jumapili, Februari 13, 2023 katika shoo ya nguvu aliyoipiga wakati wa mapumziko ya fainali za Super Bowl katika Uwanja wa State Farm, Glendale, Arizona nchini Marekani.
Baada ya mwanadada huyo kupanda jukwaani na kuanza kuperform, watu wengi walishtushwa na mwonekano wake mpya ambapo alionekana kuwa na tumbo kubwa, akiwa anaendelea na shoo ndipo alipotangaza rasmi kwamba yeye na mpenzi wake, Asap Rocky wanatarajia mgeni, kisha akalishika tumbo lake na kusababisha uwanja mzima kulipuka kwa shangwe.
Rihanna alijifungua mtoto wake wa kwanza, Mei 13, 2022.