×

Jean Baleke na Clatous Chama Wakabidhiwa Waarabu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amefichua kuwa, wamekuwa katika maandalizi mazito kuelekea katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca huku wakitoa program maalum kwa wachezaji wa timu hiyo wakiwemo Jean Baleke na Clatous Chama kwa lengo la kuhakikisha wanapata ushindi.

Simba wanatarajia kujiandaa na mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya Raja Casablanca kutoka Morocco watakaocheza Februari 18, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Jean Baleke

Akizungumza na Spoti Xtra, Mgunda alisema wameona madhaifu ya kikosi hasa washambuliaji wao kwa kutokuwa makini na utulivu, hivyo wanapokuwa kwenye mazoezi kuwapa program maalum ikiwemo kuwajenga kisaikolojia kabla ya mchezo huo.
“Ni mechi ngumu na ushindani mkubwa ukizingatia tumetoka kupoteza lakini tuko nyumbani na tunahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo dhidi ya Raja Casablanca, inatulazimu safu ya ushambuliaji kuwa na umakini na utulivu kichwani kwa washambuliaji wetu ili kufikia malengo ambayoni kukusanya pointi tatu kila mechi za nyumbani.
“Wapinzani wetu ni timu nzuri, lakini tunatarajia kupata matokeo mazuri katika ardhi ya nyumbani, ninaimani wachezaji wetu wako vizuri na tunaendelea na maandalizi katika mchezo wetu huo,” alisema Mgunda.

Stori na Ibrahim Mussa

TUNDU LISSU AIBUA MAPYA – ”VYUMA VIMEKAZA, CCM NILIACHANA NAYO NILIPOJIUNGA CHUO KIKUU”

Leave a Comment