
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), limesema kuwa litamfungulia mashtaka ya jinai rais wake wa zamani Sepp Blatter, kwa kuliingizia hasara shirikisho hilo kwa maamuzi yake ya kufungua makumbusho ya soka ‘FIFA World Football Museum’ jijini Zurich, Uswisi.
Mwanasheria wa Blatter amesema mpango huo haukuwa mawazo binafsi ya Blatter bali ni uamuzi wa FIFA ambapo kiasi cha Pauni milioni 267.8 kilitolewa kama kodi ya pango hadi 2045.