×

Pilsner ‘Kapu la Wana’ Yafanya Droo Ya Kwanza

Washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner Lager ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ inayoendeshawa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), wakionyesha zawadi zao wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika mkoani Mwanza siku ya Jumamosi. Kushoto ni Neema Abdallah, (mshindi wa televisheni), kulia ni Neema Mathias (mshindi wa pikipiki), wa pili kulia ni Hassan Joel (mshindi wa simu).Makabidhiano hayo yalifanywa na Meneja Masoko wa SBL kanda ya Ziwa, Ronald Lyatuu (wa pili kushoto).

Dar es Salaam, Jumatatu Februari 13, 2023: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imefanya droo ya kwanza ya promosheni yake pendwa ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kubainisha washindi wa kwanza wa promosheni hiyo ambayo ni maalumu kwa wateja wa bia hiyo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini.

Kupitia promosheni hiyo inayofanyika kwa muda wa wiki 8, wateja wa bia ya Pilsner watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo, televisheni, simujanja, pikipiki na zawadi ya mwisho ya gari.

Droo iliyofanyika jana, walipatikana washindi 7 kutoka kanda zote tatu, ambapo mshindi mmoja kutoka kanda ya Ziwa alishinda pikipiki, wengine watatu kutoka kanda zote tatu walishinda simujanja na wengine watatu walishinda televisheni. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18 mwezi huu.

Washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner Lager ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweries ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kutokea kanda ya Kaskazini wakionesha zawadi zao zikiwemo televisheni na simu janja baada ya hafla ya makabidhiano ya zawadi hizo yaliyofanyika siku ya jumamosi bar ya Kili time mjini Arusha.

Washindi walioshinda simujanjani Agatha Mvwango, Eli Elias na Hassan Joel; waliojishindia television za kisasani Justine Mwaipaja, Neema Abdallah na Selina Panga. Na mshindi wa bodaboda ni Neema Mathias kutoka kandaya Ziwa.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando alisema, droo hiyo ni mwanzo tu wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, akitoa wito kwa wateja wa bia ya Pilsner mikoa ya kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki kwenye promosheni hiyo kwani zawadi ni nyingi.

“Kupitia promosheni hii tunawazawadia wateja wetu wachapakazi, na zawadi zipo nyingi sana hivyo nawatia moyo wateja wetu wa mikoa ya hizi kanda tatu, yani kandayaZiwa, Kusini na Kaskazini waendelee kununua bia ya Pilsner, wapate kadi ya kukwangua, wakipata namba wataituma kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 baada ya hapo watapokea ujumbe mfupi kudhibitisha ushiriki, “alisema Marando.

Kwa upande wake, Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgafi aliwapongeza washindi wa droo hiyo ya kwanza kwanjia ya simu, na pia aliipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kufanya promosheni kwa kufuata kanuni na taratibu za bodi ya Michezo ya kubahatisha.

Hii ni maraya pili bia ya Pilsner imekuja na promosheni hii ya ‘Kapu la Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni kwa washindi 22 wa kampeni hiyo.

Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na:

Rispa Hatibu

Meneja Mawasiliano, SBL

Simu: 0685 260 901

Barua Pepe: [email protected]

Leave a Comment