×

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi  Afungua Ubalozi Mdogo wa UAE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)  akiongozana na viongozi kutoka Ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto)  akisalimiana na moja ya viongozi kutoka Ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  akifungua kitambaa kuashiria zoezi la uzinduzi wa Ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni huo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  amefungua Ubalozi mdogo wa Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), hoteli ya  Park Hyatt Shangani ,Zanzibar.
Halfa hiyo  imehudhuriwa na Waziri wa Nchi anaeshughulikia Mambo ya nje Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Shakhboot Bin Nahyan Alahyan, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi ,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga, Balozi mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Zanzibar Saleh Ahmed na Viongozi wa chama na Serikali .

Leave a Comment