
Wakati Machi 3, 2023 Klabu ya Soka ya Mapinduzi FC ikitarajia kujitupa uwanjani kumenyana na Klabu ya Soka ya Azam FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 16 bora, Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mussa Magogo amesema klabu yake imejipanga kuhakikisha inapata matokeo katika mchezo huo uliopangwa kluchezwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Mgogo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Toto Africans, Pamba FC na Mwamuzi mstaafu amesema timu yake imejipanga kuhakikisha inapata matokeo katika mchezo huo” iko wazi kwamba klabu ya Azam ni miongoni mwaka klabu kubwa hapa Tanzania na kuelekea mchezo wetu na wao tumejipanga kupata matokeo mbele yao.”
“Tupo kambini kwa muda wa miezi miwili hiyo yote ni kuhakikisha tunajiweka fiti ili mchezo huo tuweze kuushinda kwani tamanio letu ni kuwa miongoni mwa timu bora nane hapa nchini ambapo tutakuwa tumeweka historia sisi kama klabu.”
Kwa Upande wake Nahodha wa timu hiyo Antony Matogolo amesema “Sisi kama wachezaji tumejipanga, kwenye kikosi tunao wachezaji wazoefu ambao kwa pamoja tukiunganisha nguvu kwa hakika tutakwenda kuonyesha ushindani kwa wenzetu wa Azam fc ambao tutacheza nao katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.”

Mapinduzi fc ni timu iliyoanzishwa mkoani Mwanza mwaka 2011 ambapo lengo lake ilikuwa ni kuleta ushindani katika ukuaji wa soka katika mkoa wa Mwanza na tangu kuanzishwa kwake klabu hiyo malengo yake ni kuona inakuwa timu tofauti jijini Mwanza ili iweze kuzipiku timu za Pamba ,Mbao, Alliance, Toto African ambazo kwa pamoja zimeshindwa kucheza ligi kuu na tangu mwaka huu.
Timu hiyo imetwaa ubingwa wa ligi ya mkoa wa Mwanza mara mbili mfululizo pamoja na kombe la utalii Cup na kwa sasa mbali na kucheza mashindano ya Azam wanajipanga kushiriki ligi ya mabingwa mikoa kwa msimu wa pili mfululizo.
Na Johnson James- GPL