×

Washindi Wa NMB “MastabataKotekote” WakabidhiwaTiketi za Kwenda Dubai

Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Phirbelt Casmir (kushoto)  akikabidhi tiketi za ndege kwa Chintan Kamania na mke wake Kaminy Chudasama pamoja na mtoto wao Eirny Kamania  baada ya kushinda bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” aliyojishindia safari ya kwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko,  Shindano hilo lilikuwa likiendeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wake wanaofanya malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia Master Card ya NMB

 

Mshindi wa droo ya “MastaBatakotekote”iliyokuwa ikiendeshwa  na Benki  ya NMb Ndugu,John Lubisha ameishukuru Benki hiyo kwa kuweka shindano hilo lililomuwezesha kuwa mshindi wa kwenda Dubai kwa mapumziko.

“Nilifurahi sana baada ya kupokea simu kwamba mimi nimekuwa mshindi, nashukuru Mungu kwa kupata hii nafasi,” amesema John Lubisha.

Aidha John ameongeza kwamba alikuwa anatumia kadi ya Nmb ya Mastercard (Kuchanja) kulipia bidhaa mbali mbali na hatimaye ameweza kupata ushindi katika droo hiyo.

Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Phirbelt Casmir akizungumza wakati benki hiyo ilipowakabidhi washindi wa bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” waliojishindia safari ya kwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko.

 

“Ili kushiriki hizi droo mshiriki anatakiwa kuwa mvumilivu kwa kuendelea kutumia huduma ya kadi( kuchanja) kwa muda mrefu na siku moja anaweza kuwa yeye ndio mshindi,” amesema Lubisha

John amewashauri Watanzania kutumia kadi ya NMB Mastercard kwani ni rahisi lakini pia ni usalama zaidi kwani kutembea na pesa nyingi(Cash) si salama kwakuwa kuna matukio mengi ya kihalifu hata hivyo kutumia Mastercard kuna rahisisha maisha.

Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Phirbelt Casmir akikabidhi tiketi za ndege kwa John Lubisha mmoja wa washindi wa  bahati nasibu ya “Mastabatakotekote” aliyojishindia safari yakwenda Dubai kwa ajili ya mapumziko

 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya kadi wa Benki hiyo Bw. Filbert Casmir  amesema washindi hao wa kampeni ya “Mastabatakotekote” iliyoanzishwa mwezi wa kumi 2022 wamekabidhiwa tiketi zao  tarehe 28 Februari 2023.

Washindi hao watalipiwa gharama zote watakazotumia Dubai ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio, hiyo yote ni kurudisha shukurani kwa wateja wa benki hiyo.

Aidha amewashauri Watanzania kuendelea kutumia Mastercard kwani benki hiyo itaendelea kuwa na kampeni mbali mbali zitakazoambatana na zawadi.

Picha ya pamoja ya washindi.

Benki ya NMB ilianzisha kampeni ya “Mastabatakotekote”  ikiwa na malengo mbalimbali ya kuhamasisha wateja wao kutumia Mastercard, kuwajali wateja wao ambapo washindi waliopatikana wanaenda Dubai kwa mapumziko.

Leave a Comment