
Klabu ya USM Alger imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa mara ya pili katika historia yao baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Zamalek SC kwenye mchezo wa fainali uliopigwa mjini Cairo.
Mchezo huo ulimalizika kwa ushindi wa 1-0 kwa Zamalek ndani ya dakika 90 kupitia bao la mapema la penalti lililofungwa na Dabbagh dakika ya tano, huku matokeo ya jumla yakisoma 1-1 na kulazimisha mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penalti.

Katika hatua ya matuta, USM Alger walionyesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kushinda kwa penalti 8-7 na kutwaa rasmi taji la CAFCC msimu wa 2025/26.
Beki wa zamani wa Simba SC, Che Fondoh Malone, ameandika historia kwa kutwaa ubingwa huo akiwa anacheza fainali yake ya pili mfululizo ya CAFCC. Msimu uliopita Malone alipoteza fainali akiwa na Simba dhidi ya RS Berkane, lakini safari hii ameonja ladha ya ubingwa akiwa na USM Alger.