×

Shikamoo JPM

IMG_0465 Moja ya baa ikiwa haina wateja.

DAR ES SALAAM: Msoto mkali! Ile tumbuatumbua majipu ya Rais Dk. Joseph Pombe Magufuli (JPM) imetajwa kusababisha mdororo usio wa kawaida kwa baadhi ya biashara nchini na kuufanya mwezi Januari ‘mwezi dume’ kuwashikisha adabu baadhi ya watu, hasa wale waliokuwa wakitegemea kupata pesa kwa njia ya ufisadi.

Baadhi ya biashara zilizokumbwa na mdororo huo zimetajwa kuwa ni zile zinazojumuisha starehe ambazo ni baa, gesti na hoteli ambazo kabla ya tumbuatumbua ya JPM zilikuwa zikineemeka kwa kujaza wateja hata mchana wakati wa kazi.

BAA HALI IKO HIVI
Jumatatu iliyopita, Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kilifanya ziara ya kushtukiza mitaani na kubaini baadhi ya baa za jijini zilizokuwa zikijaza wateja kwa sasa zikiwa tupu, zingine zikiwa na wateja wachache.

IMG_0477

Baa ikiwa na viti vitupu bila ya wateja.

Katika hali ya kudadisi, OFM iligundua hata wateja hao wachache ni wale walioingia kwa ajili ya chakula cha mchana kisha kuondoka na si vinginevyo. Baa hizo ni za Sinza, Shekilango ‘Dagaadagaa’, Magomeni, Buguruni na Kinondoni.

HOTELINI NAKO
Mbali na baa hizo, OFM ilizungukia hoteli za maeneo hayo na kujionea uhaba wa wateja huku kumbi za mikutano zikiwa wazi kutokana na uhaba wa tenda za vikao vya idara mbalimbali za serikali ambazo awamu hii zimepigwa stop kama si marufuku kwa ajili ya kubana matumizi.

IMG_1866

Vyumba vya gesti vikiwa vitupu.

GESTI NAFASI ZIPO
OFM iliendelea kupiga mzigo, ilibaini pia hali ya kipekee kwenye gesti nyingi za maeneo hayahayo baada ya kukuta vibao vimegeuzwa na kusomeka ‘NAFASI ZIPO’ au ‘VYUMBA VIPO’.

Ni tofauti na kabla kwani uchunguzi unaonesha miezi michache nyuma, gesti hizo zilikuwa zinajaza muda wote kiasi kwamba hata wateja waliokwenda mchana wa jua kali hawakupata nafasi.

IMG_20160104_133552WAHUDUMU WACHEZA KARATA
Pia OFM iliwakuta baadhi wa wahudumu katika baadhi ya gesti wakicheza karata hali iliyoonesha kuwa hakuna kazi zilizokuwa zinafanyika ili kuwafanya wawe bize.
“Kwa kweli hali si nzuri, miezi michache nyuma mida kama hii ya saa tisa alasiri, vyumba vyote vilikuwa vimejaza nyomi lakini tangu Magufuli aanze tumbua majipu kwetu hakieleweki.

“Nadhani watu walikuwa wana pesa za mchezo tofauti na sasa za mshahara, kwa hiyo lazima kubana matumizi. Nampa shikamoo Magufuli,” alisema mhudumu mmoja wa gesti iliyopo Sinza na kujitambulisha kwa jina moja la Amina.

pombe2BEI ZAPOROMOSHWA
Kutokana na hali hiyo, OFM ilibaini baadhi ya hoteli na gesti zimeamua kukabiliana na msoto huo kwa kuporomosha gharama zake huku zile ambazo zimegomea kupunguza bei zikizidi kukiona cha moto kama si cha mtema kuni.

1 Comment

  1. JPM Baba tunyooshee watu.gepu lilikuwa kubwa sana kutoka kwa aliye nacho na asie nacho.Big Up sana Mkuu.wanaendelea kuisoma namba .JPM umejipanga natulio chini tutakusaidia.Hapa Kazi tu.

Leave a Comment